Memphis Depay Mbioni Kufanyiwa Vipimo Vya Afya


Mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Uholanzi Memphis Depay ametua mjini Lyon nchini Ufaransa, tayari kwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha usajili wa kujiunga na Olympic Lyon.
Mshambuliaji huyo amethibitisha kuwasili mjini Lyon, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, baada ya uongozi wa klabu ya Man Utd kuthibitisha kumalizana na upande wa pili kwa dili la Pauni milioni 16, ikitokea Pauni milioni 21.75.
 Image result for Memphis Depay
Baadae hii leo Depay anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya, na kama atafanikiwa kufaulu mtihani huo, atasaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Olympic Lyon ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa (Ligue 1).
Depay mwenye umri wa miaka 22 anaondoka Old Trafford, baada ya kuwa na wakati mgumu wa kucheza katika kikosi cha kwanza kwa msimu huu wa 2016/17.
Anacha histoari ya kucheza michezo 16 kama mchezaji wa kikosi cha kwanza tangu aliposajiliwa klabuni hapo mwaka 2015 akitokea PSV Eindhoven.
Post a Comment
Powered by Blogger.