Memphis Depay Afunguka Haya Kuhusu Jose Mourinho

http://i0.wp.com/dar24.com/wp-content/uploads/2017/01/Memphis-Depay-Lyons-new-Dutch-forward-.jpg?resize=1200%2C630
Mshambuliaji mpya wa klabu ya Olympique Lyon ya nchini Ufaransa Memphis Depay, kwa mara ya kwanza amezungumzia mahusiano yake na Jose Mourinho.

Depay alikamilisha mpango wa kujiunga na Olympique Lyon mwanzoni mwa juma hili, na tayari ameshacheza mchezo mmoja akiwa nchini Ufaransa, amesema hakuna na tatizo lolote na Jose Mourinho.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Uholanzi, amesema taarifa kadhaa zilizoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari, alikua akiziona na kuzisoma kila kukicha lakini aliamua kukaa kimya kwa kuamini ilikua njia sahihi.

Amesema tangu Jose Mourinho alipiowasili Old Trafford mwanzoni mwa msimu huu, alikua na mahusiano mazuri na wachezaji wake wote, na aliheshimu maamuzi ya meneja huyo ya kuamuru nani acheze, na nani asicheze.

Depay, alidaiwa kuwa na matatizo binafsi na Jose Mourinho, na hali hiyo ilikua chanzo cha kushindwa kuchezeshwa katika kikosi cha kwanza akiwa Old Trafford.
Powered by Blogger.