Melody Mbassa: Najisikia Raha Kufanya Muziki Wa Dansi, Sina Wazo La Kuingia Kwenye Bongo Fleva


Hit Maker wa 'Nikukoleze', Melody Mbassa ambaye kwa sasa ameingia kwenye muziki rasmi, amefunguka na kusema kuwa hana wazo la kuingia kwenye muziki wa Bongo Fleva kwakuwa muziki wa dansi upo damuni sana, kwa sababu anajisikia raha sana kufanya 'Live Music'.

Melody alisema kuwa hana wazo la kufanya muziki wa Bongo Fleva kwa kuwa wasanii hao kutoka kwao nikwaharaka sana, pale msanii anapotoa ngoma kali na kufanya vizuri katika baadhi ya redio mbalimbali nchini, pia alidai muziki wa dansi upo damuni kuliko kufanya muziki wa kutengeneza studio.

"Kwa kweli sina wazo hilo.. hata mimi najishangaa kwa sababu naona muziki wa dansi upo damuni sana sababu najisikia raha kufanya 'Live music' kuliko nikifanya muziki ambao naenda tu kutengeneza studio na kutumia effect. Ndio maana unaona hata hii nyimbo yangu nikukoleze, ni safari yangu toka nikiwa mdogo, maana yake hii ni safari ambayo nimeianza upya, na hata ukisikiliza nyimbo yangu utasikia vyombo vya live". alisema Melody kwenye kipindi cha Afrotz cha Radio One.


Aliongeza, "Hapo utaona mimi ni mwanamuziki ambaye nafanya kitu fulani kwenye muziki huu, maana yake ni kwamba nina hamu na huu muziki. Mimi napenda kusema kwamba 'I want to be legend' wa Tanzania, yani natamani sana maana yake nawasikiliza sana wakina Marijani walivyokuwa wanafanya". 

Mbali na hilo pia mtangajazi wa kipindi hicho, Zomboko, aliweza kumpa pongezi zake kutoka kwa king of the best melody, Christian Bella mara baada ya kuisikia ngoma hiyo 'Nikukoleze'.

"Ndio maana hata Bella alipousikia huu wimbo, akili yake ilimkaa sawa, alisema kweli huyu kijana anauwezo, kweli huyu ni Melody.. kwa sababu alisikia melody yako na kuipata vizuri sana. Akanambia bwana huyu kijana ana uwezo wa kuimba". alisema mtangazaji wa kipindi hicho, Zomboko.

Hayo nimachache kati ya mengi aliyoweza kufunguka Melody Mbassa kwenye interview yake, Radio One. Unaweza kusikiliza Full Interview hapa chini.

  
Powered by Blogger.