Mbwana Samatta Aweka Wazi Jinsi Alivyopiga Kura Kwenye Tuzo Za FIFA Za Mchezaji Bora Wa Dunia 2016

Image result for mbwana samatta
Tuzo ya mchezaji bora wa Dunia inaandaliwa na shirikisho la Mpira wa miguu Duniani FIFA na wachezaji watatu wanaoingia kwenye kinyang’anyiro hicho hupigiwa kura na Makocha wa timu za taifa, Marais vyama vya mipira na Manahodha wa Timu za Taifa.


Sasa nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta yeye alipiga kura kama ifuatavyo kwenye kura ya mchezaji bora wa Dunia alimpigia..

1: Lionel Messi mchezaji wa Barcelona

2: Cristiano Ronaldo kutoka klabu ya Real Madrid

3: Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid.


Hatimae Mchezaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo alishinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia ya FIFA.

Ronaldo, 31, amewapiku Lionel Messi wa Barcelona na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid katika sherehe zilizofanyika mjini Zurich, Uswisi.
Post a Comment
Powered by Blogger.