Masoud Kipanya Anyoosha Maelezo Kuhusu Katuni Ya 'Mwamba Ni Mwamba Tu' Ya Joh MakiniIkiwa leo ni Jan 25, Mkali kutoka Kaskazini Joh Makini, amedropisha ngoma yake mpya "Waya" na kupokelewa vizuri na mashabiki zake pia kupata maoni mazuri juu ya ngoma hiyo.

Kabla ya ngoma hiyo kuachiwa hii leo, siku ya jana ilizagaa post ya 'katuni' kwenye mitandao ya kijamiii hasa Instagram inayo onyesha Jamaa akiwa anahangaika kuusukuma mwamba hadi kumpelekea kutoa hewa chafu na mwisho anaonekana Masoud Kipanya akifunguka kwamba 'Mwamba ni Mwamba Tu', cha kufahamu ni kwamba Idea hiyo imetolewa na Joh Makini.

Masoud Kipanya alifunguka na kusema kwamba Joh alimcheki na kumtaka kufanya kitu cha tofauti kwa kumtaka amtengenezee katuni ambayo inaonyesha mtu anausukuma mwamba lakini mwamba asiouweza, alafu pembeni kipanya aseme maneno hayo.
“Unajua Joh aliniambia Brother mi nataka tufanye kitu cha tofauti, akasema kwamba nataka unitengenezee katuni ambayo inamuonyesha mtu anausukuma mwamba lakini mwamba asiouweza alafu pembeni kipanya aseme maneno hayo, sio kwamba nilifikiria mimi". alisema kwenye XXL ya CloudsFm.


Aliongeza, "Sasa jinsi nilivyoielewa concept yake yaye ni kwamba Joh Makini ni mwamba sasa anayesukuma ni nani hapo ndio sielewi, kwasababu yeye aliniambia borther nichoree mchoro uko hivi, hivi.. sasa si unajua hawa ni ma-artist wanacompetition kila mtu anakuwa anajaribu kutengeneza idea yake, mtu anajaribu kutengeneza statement yake kwamba yeye ni bora.. sasa kitu kizito na ile ni hewa tu imetoka sio kujamba ni hewa tu"
Powered by Blogger.