Mashabiki Wa Arsenal Waguswa Na Ujumbe Huu Wa Alexis Sanchez


Mashabiki wa klabu ya Arsenal wamemuangukia mshambuliaji Alexis Sanchez kwa kumtaka asichukue maamuzi ya kuondoka klabuni hapo, baada ya kuandika ujumbe mzito kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram.

Mashabiki wa Arsenal wanaomfollow mshambuliaji huyo, walionyesha kushtushwa na ujumbe uliandikwa na Sanchez katika ukurasa wake, ambao unasomeka hivi kwa lugha ya kingereza "Strong people smile with a broken heart. They cry with the doors closed and fight battles that no one knows."

“Watu wazito wanacheka huku wakiwa wamevunjika moyo. Wanalia huku milango ikiwa imefungwa na wanapigana bila ya muhisika kuwajali.”

Mashabiki wa Sanchez kwa nyakati tofauti walitoa maoni yao kuhusu ujumbe huo, na wengi wao walionyesha hisia ya kuguswa na maneno alioyaandika mshambuliaji huyo.


Asilimia kubwa ya mashabiki, walimtaka asifanye maamuzi magumu ya kuondoka klabuni hapo, na badala yake aendelee kuwatumikia hadi watakapofikia hatua ya kufurahia mataji.

Mshambuliaji huyo amewaweka mashabiki wa Arsenal katika hali ya sintofahamu kuhusu uhusiano wake na Arsenal Wenger, ambapo zaidi ya mara moja amekua akionyesha vitendo vinavyopingana na mzee huyo.

Sanchez alionyesha unyonge baada ya kutolewa nje ya uwanja wakati wa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita, ambapo Arsenal walipambana na Swansea city na kuchomoza na ushindi wa mabao manne kwa sifuri.
Post a Comment
Powered by Blogger.