Martin Kadinda Atoa Pongezi Hii Kwa Wema, Adai 'Amebadilika Hadi Raha'


Aliyekuwa Meneja wa Mrembo wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Martin Kadinda, amempongeza mwanadada huyo kwa kubadilisha mfumo wa maisha yake.
Martin amesema hayo jana, ambapo ameeleza  kuwa pongezi zimuendee bidada huyo kwa kitendo alichoamua kufanya kuhusiana na maisha yake kutoyachoresha kwenye jamii kwa kuamua kufuta picha zake zote kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii. Kwa hatua hii anahitaji pongezi.
”Uamuzi alioufanya Wema ni mzuri na wa kupongezwa, mimi na familia yake hatukuwa tukipendezewa nayo kwa kuwa ilikuwa ikichafua jina lake,” ameeleza Martin kwenye mahojiano na mtanzania.

 Wema Sepetu
Martin ameongezea kwamba Wema ambaye amebadili meneja kwa sasa, "amekuwa tofauti na alivyozoeleka maana amekuwa muelewa na msikivu kwa anachoelezwa".
Wema alichukua maamuzi hayo mara baada ya kuingia mwaka mpya 2017, kufuta picha zake zote bila kutoa sababu ya msingi iliyompelekea kuchukua hatua hiyo, Kila mtu alihoji kwa namna aliyoweza na kufikiria yeye lakini hakuna aliyepata majibu sahihi kwani mrembo huyo naye hakuwa tayari kuzungumzia swala hilo.
Ukimya huo umetanda hadi leo ukiwa na maana kuwa Wema Sepetu alimaanisha kwa alichokifanya hatua amabayo impelekea Martin Kadinda kumpa pongezi, kwani hatua hiyo imeleta matokea mazuri hadi sasa hakuna skendo wala ishu yoyote mbaya inayoendelea juu ya bidada huyo.
Post a Comment
Powered by Blogger.