Man City Kuwasha Moto Na Tottenham Etihad


Mshambualiaji Gabriel Jesus ameruhusiwa kucheza katika mechi dhidi ya Tottenham baada uhamisho wake wa pauni milioni 27 kutoka klabu ya Palmeiras kukubaliwa rasmi siku ya Alhamisi.

Fernando huenda akarudi baada ya jeraha lakini kiungo wa kati Fernandinho bado anahudumia marufuku.

Beki wa Tottenham Jan Vertonghen anatarajiwa kukosa kushiriki katika kipute hicho baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu ambalo litamweka nje kwa wiki sita.

Kiungo wa kati Erik Lamela atasalia nje kutokana na jeraha la nyonga.
Post a Comment
Powered by Blogger.