Madee Afunguka Juu Ya Tuhuma Za Uporaji Wa Simu 'S4'
Msanii wa bongo fleva Madee amesema hajutii matusi yanayotukanwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa amepora simu kwa kuwa wanaomtukana hawaujui ukweli na wakiujua watatulia.
Madee amesema hajapora simu bali alikuwa anadai pesa ambayo aliitoa kwa ajili ya kufanyiwa kazi na badala yake haikufanyika jambo lililomfanya aende kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya kurudishiwa pesa yake, na ndipo hayo yakatokea.
"Baada ya kuona pesa yangu ipo tu imekaa
hafanyi kazi yoyote, nikafuatailia sheria, nikaenda polisi, nikasaidiwa
kupata haki yangu, nashukuru nimepata haki yangu, wala sijutii
kinachoendelea, sasa mi naweza kupora simu rafiki yangu, mi natumia simu
yangi iPhone 7 na hiyo simu nayoambiwa nimepora ni S4, halafu kama ni
kupora nisingeenda na polisi" amefafanua Madee kwenye eNewz
Pia Madee amesema pesa yake huwa haipotei hata kama ikiwa imechukuliwa na maiti.
Hata hivyo Madee amesema uongo huwa
hauishi muda mrefu hivyo hawalaumu wale ambao wamemtukana kwa kuwa
hawaujui ukweli na anaamini kuna siku watu wote wataujua ukweli.