Lulu Diva: Bora Hata Ingekuwa Kutongozwa Lakini Mimi Najutia Kuwa Video Queen
Video Queen Lulu Diva ambaye sasa ameanza kufanya muziki wa bongo fleva amefunguka na kusema anajutia maamuzi yake kuingia kwenye tasnia, kama video queen katika video mbalimbali za wasanii na kusema kazi hiyo imekuwa haiheshimiki.
Lulu alisema anajutia kuingia kwenye fani hiyo kwani imekuwa ikiwashushia heshima kutokana na baadhi ya video queen kufanya mambo ya ajabu katika jamii jambo ambalo linawafanya watu kuona wote wapo sawa.
"Ni bora hata ingekuwa
kutongozwa lakini mimi najutia kuwa video queen kwa sababu kuna baadhi
ya video queen wamekuwa matendo mabaya, wanapiga piga picha za uchi
hovyo, na namna wanavyoishi katika jamii wanapelekea watu wote kuona
kuwa Video queen ni watu wenye tabia mbovu" alisema Lulu Diva kwenye Planet Bongo.
Mbali na hilo Lulu Diva alisema kuwa
kazi hiyo pia haina maslahi yoyote yale kwani pesa wanazopewa na wasanii
ni pesa kidogo sana ambayo haiwezi kuwafanya kupiga hatua yoyote ile
"Wasanii wanatakiwa kujua umuhimu wa
video queen maana ni muhimu lakini pesa wanazokuwa wanawapa video queen
ni ndogo sana na hailingani na kazi ambayo wanakuwa wamefanya kwenye
video zao" alisisitiza Lulu Diva