Lile Pambano La Soulja Na Chris Brown Huenda Likatokea Kwa Meek Mill Na Drake, Meek Afunguka Haya


Ikiwa bado siku kadhaa kufanyika kwa pambano la Chris Brown pamoja na Soulja Boy, hatimae Meek kaja na hii mpya kwa kutangaza kama hasimu wake wa siku nyingi.

Meek Mill anawaunga mkono Chris Brown na Soulja Boy baada ya kutangaza kuwa watapambana ili kuonesha uwezo wao wa nani mkali kati yao.

Kupitia video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Meek Mill amesikika akisema hata yeye yupo tayari kupigana na Drake endapo atapewa Dola Milioni 5 za kimarekani ambazo ni sawa na Tsh Bilioni 10.

Marapa hao wawili tangia mwaka jana wapo kwenye Bifu kali mpaka sasahivi, Bifu ambayo kwa kiasi kikubwa lilichochewa na mrembo Nicki Minaj baada ya kuingia kwenye mahusiano na Meek Mill.

Hii hapa video hiyo


Post a Comment
Powered by Blogger.