Licha Ya Kumdis Joh Makini, Msodoki Ataja List Ya Wasanii 3 Wakali Wa Hip Hop Bongo Joh Akiwemo


Rapa Young Killer ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Sinaga swaga' amefunguka na kutaja wasanii wa Hip hop bongo wakali ambao yeye anawaheshimu na kuheshimu kazi zao siku zote.

Young Killer alimtaja Prof Jay kuwa ndiye Rapa namba moja kwake, akamtaja Fid Q kuwa ni rapa namba mbili kwake huku namba tatu ikieenda kwa Joh Makini ambaye amemdiss kwenye wimbo wake huo mpya kuwa anabebwa na vyombo vya habari.


"Watu wameni tafsiri vibaya kuhusu Joh Makini na mstari wangu ule. Joh Makini ni brother na anafanya kazi nzuri sana binafsi nampenda na kumuheshimu na katika top three yangu ya wanamuziki wa Hip hop bongo Joh Makini yupo, wa kwanza ni Prof Jay, wapili ni Fid Q na msanii wa tatu wa Joh Makini". Alisema Young Killer kwenye Friday Night Live jana usiku.
Post a Comment
Powered by Blogger.