Kutana Na Viatu Vya Kijanja Vyenye Uwezo Wa Kubadilika Kuendana Na Muonekano UnaoutakaUnaambiwa Teknolojia inakua kila kukicha na nina weza kusema mwaka 2017 tutarajie kujionea makubwa kwani wanasayansi wanazidi kuturahisishia mambo yenye ugumu hata kwa kutazama tuu.

Anayway Jana nchini Marekani Wanasayansi wametengeneza viatu visivyochakaa, unaweza ukajiuliza kutokuchakaa kunatokana na nini?jibu ni rahisi tu ni kwamba utakuwa na uwezo wa kubadilisha rangi ya viatu hivyo pale tu utakapohitaji aina yoyote ile ya rangi,na kingine ni kwamba utakuwa unapata notifications zote zinazoingia kwenye simu yako kupitia kiatu hicho kwa ku’vibrate na pia kitakuwa na uwezo wa kukuunganisha na rafiki yako kwenye mitandao ya kijamii kwa kugusana tu miguu yenu.

Viatu hivyo vya aina ya Snekers Vixole v10 vinaendeshwa kwa simu (smartphone)  kupitia App maalumu ambayo inapatikana kwenye mfumo Android na iOS.

Ili kuwezesha viatu hivyo kuweza kubadilika ni kwamba Ngozi yake ya nje imetengenezwa kwa mfumo wa kioo cha LED ambacho kinasaidia kiatu hicho kubadilika kadri utakavyo.

Mmiliki wa viatu hivyo atakuwa na uwezo wa kubadilisha rangi aipendayo kama Wallpaper,Maua,Rangi na kuweka urembo wowote anaoutaka kwa kutumia simu yake ya mkononi,na kuhusu chaji viatu hivi vitakuwa na Battery maalumu ambayo itadumu kwa masaa nane ukiwa umeichaji Full.

Viatu hivi vipo tayari na vinatarajia kuingia sokoni mwezi June mwaka huu na gharama yake itakuwa ni Dola $160 sawa na Tsh 350,000/= kwa pesa ya Madafu lakini bila gharama za ushuru na usafirishaji.

Tazama video ya kiatu hicho hapa chiniPost a Comment
Powered by Blogger.