Kanye West Na Familia Yake Wazuru Kwenye Kaburi La Marehemu Mama Yake ‘Donda’


Kwa kile kinachoonekana kama mapumziko marefu baada ya kupatwa na matatizo ya msongo wa mawazo Rapa Kanye West na Kim Kardashian juzi walichukua ndege Binafsi iliyowatoa Los Angeles wanakoishi kwa sasa mpaka nyumbani kwa Familia ya Kanye West jijini Oklahoma.


Watoto wao North West na Saint ni mara yao ya  kwanza kutembelea familia ya Baba yao iliyopo jijini Oklahoma kwani hata hivyo walipata nafasi ya kuzuru kwenye kaburi la Bibi yao (mama yake na Kanye West) pamoja na kusalimiana na ndugu wengine.

Hata hivyo Jarida la Metro Entertainments limedai wawili hao hawakuchukua muda mrefu kwani jana jioni walirejea Jijini Los Angeles kuendelea na maisha yao ya kawaida.

Mbali na hilo pia tumeweza kuona Kim Kardashian kurejea tena kwenye mitandao ya kijamii Jumanne hii baada ya kuisusa kwa miezi mitatu na katika kipindi ambacho kumekuwepo na tetesi za mgogoro kwenye ndoa yake na Kanye West.


Kim pia ameupdate app yake kwa kuweka video akiwa na mume wake Kanye pamoja na watoto wao wakifurahia muda bora pamoja.

Post a Comment
Powered by Blogger.