Kanye West Mbioni Kuachia Ngoma Mpya Kwa 'Surprise'


Ni ngumu kumtenganisha Kanye West na muziki. Kwa mujibu wa ripoti ya E Newz, rapper huyo ameanza kupika kazi mpya wakati akiendelea na matibabu.

Kanye West anajiandaa kuvunja ukimya kwa surprise. Chanzo kilicho karibu na rapper huyo kilipiga story na mtandao wa E Newz, nakudai  kuwa rapper huyo yupo chimboni kuandaa nyimbo mpya atakazitoa kwa kushtukiza. Pia anajiandaa na show kadhaa katika msimu wa kiangazi.

Kimedai kuwa Yeezy anafanyia kazi nguo zake mpya pamoja na collabo kadhaa. West amedaiwa kutengeneza muziki tangu November mwaka jana aliporuhusiwa kutoka hospitali alikokuwa akitibiwa na tatizo la uchovu na matatizo ya akili.

Kwa sasa anaendelea kupona kwa msaada wa familia yake hususan mkewe, Kim Kardashian. Vyanzo vinasema watoto wake amewapa kipaumbele zaidi kwa sasa na anataka kuwa kuwa baba mwema.

Mbali na hilo pia ametengeneza studio ya muda kwenye jumba lake la kifahari la Bel-Air ili awe na muda wa faragha anaohitaji ili apone kabisa wakati pia akitengeneza muziki mpya.

Vyanzo vilidai kuwa Kanye anafananisha kilichomtokea kama ajali mbaya aliyowahi kuipata pamoja na kifo cha mama yake. Vimsema anajisikia kutengeneza nyimbo kama zile zake bora zikiwemo “Through The Wire” na ‘808s’ baada ya masahibu hayo.

Post a Comment
Powered by Blogger.