Kalapina Atoa Ushauri Huu Kwa Wanao’post Picha Za Chid Benz Na Nando Mitandaoni


Ni wiki sasa imepita tangia kusambaa kwa picha za Rapa Chid Benz na mshiriki wa Big Brother Africa Nando kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonesha wakiwa wamechoka kiafya huku stori zikiwa ni wamerudia kutumia madawa ya kulevya.Sasa leo msanii wa hip hop ambae pia ni Mwanaharakati wa kusaidia walioathirika na Madawa ya Kulevya Kalapina kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio amesema

Mimi nawaunga mkono watu wote wanaoweka picha hizo mitandaoni kwani zina raise awareness kwenye jamii na hii itasaidia watu kujua ukubwa wa tatizo hili kwani Nando na Chid hawa ni wachache tu kwavile hawa wanajulikana ila wangapi wanaotumia ambao hawajulikani? Hili ni tatizo la jamii nzima

Picha za Chid Benz zimekuwa gumzo mitandaoni kwani mkali huyo wa Dar es Salaam Stand up alipelekwa Rehab na Babu Tale lakini alivyorudi kitaani kuna tetesi zinadai mkali huyo karudia tena kutumia Ngada.Melody Mbassa - Nikukoleze (Official Music Video)


Post a Comment
Powered by Blogger.