Insta Pamewaka!! Nay Wa Mitego Amuwashia Moto Madee, Adaiwa Kumdiss Kwenye Ngoma Yake ‘Hela’


Wafalme wa Manzese, Madee na Nay wa Mitego, wameirejesha tena bifu yao. Bifu hiyo imerudi upya baada ya Madee kuandika mstari kwenye wimbo wake mpya, Hela ambao umetafsiriwa kumwendea hasimu wake, Nay.

“Yule kijana wa home sio staa, anatukana hata waliomzaa, wivu tamaa na njaa ukiendekeza ujue kidole utakaa,” Madee amerap kwenye wimbo huo.

Baada ya muda mfupi tangu wimbo huo utoke, Nay aliandika kwenye Instagram, “Leo nimesikia Wimbo Mbayaaaaa kuliko nyimbo mbaya nilizowahi kusikia Mwaka huu.” “Mtag uyo Msanii mwenye huo wimbo Kama ushausikia..?!”

Unaweza kusikiliza ngoma hiyo hapaMbali na diss hiyo ya Madee kwa Nay wa Mitego, mnano mwaka 2013 pia Nay wa Mitego alichafua hali ya hewa kwa kutengeneza mijadala kwenye radio na kwenye mtandao kwa ngoma yake, Salam Zao.

Kwenye Salam Zao, Nay aliweza kufanya kile akifanyacho kwa uzuri (do what he does best) kuponda.

Kupitia ngoma hiyo hiyo, Salam Zao, Nay alianza kwa kumdiss Madee kwa kusema kuwa yeye ndio rais wa Manzese na kwamba Madee amesanda. “Mi ndo rais wa Manzese yule tozi kasanda, Manzese mikono juu naiongoza kamanda,” anachana Nay.
Post a Comment
Powered by Blogger.