Huu Hapa Ujumbe Wa Paul Makonda Kwa Fid Q Kuhusu Ngoma Yake 'Roho'


Ni mara chache hutokea viongozi wa Serikali kuandika au kufatilia muziki wa kizazi kipya na kukubali ikiwa pamoja na kuonyesha hisia zake waziwazi.

Leo Jan 20, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mh Paul Makonda amepost video ya wimbo wa Fid Q aliomshirikisha Christian Bella unaoitwa "Roho".


Baada ya kupost kipande cha video hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaan, Paul Makonda ameandika "Hakika umetubeba hakuna bingwa na mbabe ktk anga hizi kama wewe, huna mbwembwe na ujumbe unafika. #Mzikimgum".

 
Post a Comment
Powered by Blogger.