Hii Hapa Orodha Ya Wasanii Ambao Mwana FA Adai Hatafanyanao Kazi


Rapa Mwana FA ambaye kwa sasa anafanya vyema na ngoma yake 'Dume Suruali' amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpango kwa sasa kufanya kazi na wasanii kama Lady Jaydee, Prof Jay, Juma Nature na wengine wengi.

Mwana FA adai kwa sasa hana mpango wa kufanya kazi na wasanii wengi tu lakini kutofanya nao kazi haina maana kuwa ana matatizo nao.


 Mwana FA

"Kwa sasa sina mpango wa kufanya kazi na Lady Jaydee, harafu hili swali limekuwa likijirudia sana sina mpango wa kufanya kazi na Prof Jay, Juma Nature na wasanii wengine wengi tu, lakini sina tatizo nao na wala sina tatizo na yoyote kati yao" alisema Mwana FA kwenye Planet Bongo.

Mbali na hilo Mwana FA anasema anafurahi kuona muziki wa hip hop nchini sasa umegeuka na kufanya vizuri zaidi kuliko hata ngoma za wasanii wa kuimba na kusema hiyo ni dalili kuwa wanamuziki wa hip hop wamegundua sehemu walipokuwa wakikosea.
Powered by Blogger.