Hatimae Van Gaal Astaafu Kazi Ya Ukocha Baada Ya Miaka 26


Meneja wa zamani wa Manchester United na Uholanzi Louis van Gaal amesema amestaafu kazi ya ukufunzi baada ya miaka 26 katika taaluma yake.

Van Gaal, 65, hajafanya kazi uwanjani tangu alipopigwa kalamu na United saa chache baada ya kushinda kombe la FA mwezi Mei 2016.

Van Gaal
 Van Gaal akiliinua kombe la FA mwezi Mei 2016- na kupigwa kalamu saa chache baadaye

"Kwa mafikira yangu nilidhani nitastaafu, nikafikiria ni mapumziko ya muda, lakini kwa hivi sasa sidhani kama nitarudi kwa kazi ya ukufunzi," Van Gaal alinukuliwa na gazeti la Uholanzi la De Telegraaf. Van Gaal pia alikuwa mkufunzi wa klabu ya Ajax, Barcelona, Bayern Munich and AZ.

Van alitangaza uamuzi wake siku ya Jumatatu baada ya kupata tuzo kuu katika taaluma yake kutoka kwa serikali ya Uholanzi kwa mchango wake katika soka.

Alisema shida za kifamilia ndizo zilichangia uamuzi wake huo, huku gazeti la De Telegraaf likisema uamuzi wake ulichangiwa na kifo cha mkwe wake mwezi Disemba. ''Mambo mengi yametokea kwa familia yangu, unakuwa binadamu kwa mara nyingine kwa kukiri ukweli,'' aliongezea Van Gaal.

Raia huyo muholanzi amesema bayana, alikataa nafasi nzuri za kuendeleza taaluma yake kwa kukataa kazi mataifa ya Mashariki ya Mbali.
Post a Comment
Powered by Blogger.