Hatimae Kinara Wa Madawa Ya Kulevya ‘el Chapo’ Apandishwa Kizimbani


Muuzaji wa Madawa ya kulevya Maarufu Duniani na raia wa Mexico Joaqin Guzman,amepandishwa mahakamani Mjini New York ili kusomewa mashtaka yanayomkabili ya uuzaji wa madawa ya kulevya, utekaji nyara na mauaji, lakini Guzman amekana mashtaka hayo yanayomkabili.

Guzman ambaye pia anajulikana kama El Chapo, alisafirishwa kwenda Marekani siku ya Alhamisi baada ya kushindwa kwenye kesi ya kutaka ashtakiwe nchini Mexico.

Aidha,Waendesha mashtaka wanamtuhumu Guzman kuwa ni mkuu wa kundi la Sinaloa, ambalo linajihusisha na usafirishaji wa viwango vikubwa vya madawa ya heroin na cocaine, na madawa mengine ya kulevya kwenda nchini Marekani.

Hata hivyo, Mawakili wa El Chapo wamedai kuwa  mteja wao hahusiki na kundi lolote la wahalifu kama inavyodaiwa na mahakama.

Guzman amejichukulia umaarufu mkubwa sana duniani kwa kazi yake ya uuzaji na usambazaji wa madawa ya kulevya ambapo alikuwa akisakwa mpaka alipokamatwa nchini Mexico na kusafirishwa Marekani kusomewa mashtaka yanayo mkabili.
Post a Comment
Powered by Blogger.