Hatimae Jennifer Lopez Athibitisha Collabo Yake Na Drake, Msikie Hapa


Jennifer Lopez na Drake wamekuwa wakitengeneza vichwa vya habari kuhusiana na tetesi za uhusiao wao. Wakati bado bado haijulikani kama kweli wana uhusiano, J.Lo hatimaye amethibitisha kuwa yeye na Drizzy walikuwa wakirekodi ngoma mpya.

Wakati akifanya promotion ya series yake ya NBC, Shades of Blue, Jenny aliulizwa kuhusu kazi ijayo na Drake.


“We did a song together,” aliiambia Entertainment Tonight. “We’ll see if it’s on his next album, but he just asked me to do a song with him and that’s what we were doing,” aliongeza.

Na katika mahojiano mengine na Extra, aliongezea kwa kusema, “We did one song together. I don’t know if we’ll do more, we’ll see.”Hivi karibuni Drake alidaiwa kumnunulia Jennifer mkufu wenye thamani ya $100,000. Inshu hii ilianza kama kiki, ni baada ya Drake na Jennifer Lopez wote kupost picha mpya kwenye mtandao wa Instagram wakiwa pamoja wakionekana ni kama wapenzi, mashabiki wakamjia juu Drake.

 

Wawili hao walipost picha hiyo huku kila mmoja akiacha bila ya kuandika chochote na kuzidi kuongeza idadi ya maswali kwa mashabiki.
Post a Comment
Powered by Blogger.