Hatimae Gerard Deulofeu Asajiliwa Na Klabu Hii

 
Mshambuliaji wa klabu ya Everton Gerard Deulofeu amejiunga na magwiji wa soka wa mjini Milan nchini Italia AC Milan kwa mkataba wa miezi sita.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Hispania, alifanyiwa vipimo vya afya jana jioni, kabla ya kukamilisha taratibu za kujiunga na klabu hiyo ambayo inapigana kurudi katika hadhi yake ya ushindani ndani na nje ya Italia.

“Gerard Deulofeu amejiunga na AC Milan kwa mkopo wa muda mfupi, atakua huko hadi mwishoni mwa msimu huu,” klabu ya Everton ilithibitisha kupitia tovuti yake.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22, aliwasili Goodison Park mwaka 2013 kwa makubaliano ya usajili wa mkopo wa muda mrefu akitokea FC Barcelona, kabla ya kusajiliwa moja kwa moja Julai 2015.

Akiwa Everton alifunga mabao manane katika michezo 75 aliocheza na inaaminika usajili wake wa mkopo ndani ya klabu ya AC Milan utakua na mafanikio makubwa.
Powered by Blogger.