Hatimae Eminem Amkubali Kendrick Lamar Kama Mkali Wa Rap Kwa Kumpa Mtego Huu

eminem-1-736x414
Mwanamuziki Nguli wa Kurap Eminem ni mmoja wa wasanii ambao mpaka akukubali kama wewe mkali, lazima uonyeshe kweli kwamba wewe ni chuta kwenye kutema cheche za kurap.

Inasemekana Eminem hakuwa anaamini mistari anayoitemaga Kendrick Lamar ni ya kwake bali alikuwa ana andikiwa na mtu.

Hii imetokea juzi kati ambapo Ed Sheeran mwanamuziki wa Uingereza, alieweka wazi kilichotokea studio Eminem na Lamar walipokutana.

Eminem alimwalika Kendrick studio, kwa sababu alisikia Lamar mkali sana kwenye mashairi Kendrick alifika studio na wanae kibao. Ila Eminem alimwambia Kendrick anamtaka yeye mwenyewe studio, producer wake atakuja kumrekodi, Ila masela wake hawatakiwi kuingia.

 Related image

 Huwa Ikifika point hii Rappers wengi huanza kutetemeka haswa kama ni wapya kwenye gemu ila kama kawa Kendrick alikuwa ametulia akakubali.

“Kendrick alitunga mistari mikali, kila mtu alipata nafasi ya kuisikiliza ndani ya studio, Baada ya hapo Eminen alisema amefanya hivyo kumjaribu Kendrick kujua kama ana andika mistari yake ama laa." Alisema Ed Sheeran

Hapo ndipo alipotambua kuwa Eminem ni mkali kwenye Game.
Post a Comment
Powered by Blogger.