Hatimae Alama Maarufu Ya 'Hollywood' Yabadilishwa Na Kusomeka 'Hollyweed'

Wakazi wa Hollywood nchini Marekani waliamka Jumapili ya jana na kukuta alama ya kihistoria ya Hollywood ikiwa imebadilishwa na kusomeka Hollyweed.

Alama hiyo ilifanyiwa hujuma na mwanaume aliyerekodiwa kwenye video za surveillance, kwa mujibu wa polisi wa Los Angeles. Mwanaume huyo alikuwa amevaa nguo nyeusi alipanda kwenye mlimani na kwenda kubadilisha alama hiyo.

Mtuhumiwa huyo aliendelea kukaa kwa muda baada ya kukamilisha uharibufu huo na kwa mujibu wa LAPD akimatwa atakabiliwa na kesi ya kuvuka sehemu isiyoruhusiwa.

Tukio hili la kubadilishwa kwa nembo hii ya Hollywood kuwa Hollyweed linadaiwa kufuata mwangwi wa jamaa mmoja  alikuwa anajulikana kama Danny Finegood ambaye ni marehemu, miaka 41 iliyopita aliwahi kuibadilisha nembo hiyo yeye pamoja na marafiki zake  Jan. 1, 1976.

download (4)


Ishu ya kubadilisha nembo hiyo ya “Hollywood” kuwa “Hollyweed” ilianza pindi California ilipolegeza kwenye sheria ya Marijuana, hakuna ushahidi wa kutosha kama tukio hili la 2017 linamaana sawa na hilo la 1976.
Post a Comment
Powered by Blogger.