Goncalo Guedes Atua Rasmi Parc des Princes

Mabingwa wa soka nchini Ufaransa, klabu ya Paris St Germain (PSG), wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa pembeni mzaliwa wa nchini Ureno Goncalo Guedes akitokea SL Benfica.

Mshambuliaji huyo amejiunga na PSG baada ya kukataa kwenda Old Trafford yalipo makao makuu ya klabu ya Man Utd siku mbili zilizopita.

Guades mwenye umri wa miaka 20, amesaini mkataba wa miaka minne na nusu ya kuitumikia klabu ya PSG.
Powered by Blogger.