Fid Q: Hata Siku Moja Usitishwe Na Msanii Kisa Ana Followers Wengi Basi Ndiyo Uamini Yeye Ndiyo Star


Kuna siku nilishawahi kujiuliza kwanini? kuna wasanii wakubwa Duniani ambao wana’followers wachache kwenye Akaunti zao za mitandao ya kijamii ukilinganisha na wasanii wa Tanzania ambao wengi wao majina yao hayajulikani hata pengine nchi jirani.

Wasanii wa kimataifa kama Mohombi,R-Kelly na wengine kibao Followers wao kwenye mtandao wa Instagram hawafiki hata Milioni 1 licha ya ukubwa wa majina na umaarufu walio nao Duniani,Wakati Tanzania wasanii na waigizaji wa Filamu karibia 12 akaunti zao za Instagram zina Followers zaidi ya Milioni 1.

Swali langu limepata jibu kutoka kwa Rapa Fid Q ambae amesema hata siku moja usije ukadanganyika kuwa msanii  kuwa na Followers wengi ni ishara ya kuwa Star dhidi ya yule mwenye Followers wachache.

Fid Q amesema Followers wengi hawa’exist kwenye real life na hata kama wana’exist basi hawapo real kwani alitolea mfano kwa kusema utakuta kuna wasanii wana’followers wengi lakini wakienda kwenye show wanachezea za uso je,hao followers wako wapi? alihoji Fid Q

 Image result for fid q

Mitandao ya kijamii isikudanganye kwenye maisha ya kawaida utakuta  kuna wasanii wengine wana followers wengi wakienda kufanya show wanachezea za uso sasa hawa followers wanaishi wapi? so ina maana followers wengi ni fake hata kama wakiwa real wengi wao hawa’exist in real life, katika maisha halisi hawapo kwasababu kama mtu una’followers milioni 2 na unaweza kufanya Event Masai Club na haujazi Followers wako wapo wapi?“Aliendelea kuhoji Fid Q

Kuwa na Followers wengi kwa msanii kwenye Social Networks haimaanishi kuwa ndiyo Star, Kwahiyo usidanganyike na suala la views sijui nini? haya ni maisha ya kwenye social networks haya’exist in real life. Numbers zipo tu pale kwa faida ya watu wa biashara kwamba huyu mtu ana’followers wengi basi tumpe atutangazie sabuni, lakini hata siku moja usitishwe na msanii heti kisa ana followers wengi basi ndiyo uamini yeye ndiyo star Nope fanya research vizuri“Alisema Fid Q kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.
Post a Comment
Powered by Blogger.