Fid Q Awashtua Mashabiki Kwa Post Hii Kuhusu Ngoma Ya Joh Makini 'Waya'Inawezekana na wewe ni miongoni mwa mashabiki wa bongofleva ambao wamewahi kuzisoma sana mitandaoni habari zilizoandikwa kwamba wawili wa HipHop Tanzania Joh Makini na Fid Q huwa wana beef.

Kuanzia mwishoni mwa mwaka jana tulianza kuona wawili hawa wakiendelea kuonyesha kwamba hawana tatizo au hakuna beef kati yao ambapo Fid Q ameendelea kudhihirisha kwamba hakuna tatizo kwa kupost leo January 26 kipande cha video mpya ya Joh Makini.


Baada ya kupost  video hiyo fupi Fid Q alisisitiza kwenye caption na kuelekeza watu waende kuitazama kwa "New video alert WAYA toka kwa Mwamba wa Kaskazini @JohMakiniTZ (link ipo kwenye BIO yake nenda kajionee Maunyama)".

Haikuishia hapo, pia Nikki wa Pili na Joh Makini waliweza kutoa comment zao kwenye post hiyo ya Fid Q.


Post hii imeibua mijadala tofauti tofauti ikiwa mashabiki wengi wameanza kuhitaji wimbo wa pamoja kati ya wakali hao wa Hip Hop nchini na kuwashauri kuandaa show ya pamoja wazunguke mikoani kuchukua pesa zao

Hizi ni baadhi ya comments:


african__worr@therealfidq: soon collabo ipo njian…..naamini itanunua viewz bila cash mkononi nice big brav @therealfidqtammy_thebaddest

mnyamwenga91: wafenyi fiesta yenu kila mkoa wewe na johmakini niamini mimi mtakuwa mabilionea

masterplanmaster: Mm snaga shidaah na nyie sema collaboration ndo hamtaki kutupatia naamin hphp nyie ndo malejendari hadi sasa mko vizur ikizngatwa wote mnangoma mpya #StayBlessed@therealfidq

yusuph.alex: Gud umetudhihirishia Huna bifu na mwamba wa kaskazin@therealfidq

sao_thimotheo: kweli kwenye group la ma mc fake admin hawez kuwa ngosha

hassanmansury: hip hop ya kweli hupigwa redion sometime maraika wa heri nao.hutembelea motoni@thanks broda ngosha

willyjozee97: Sana ngosha charles_daniel_:makena Tusikatishane tamaa,kama unaona mbovu imba yako!tuwasapoti wasanii wetu big up @therealfidq na we @johmakinitz msapoti mwenzako ka yy alivyo onyesha sapoti kwako

kimaromweusi: Sarut Ngosha nimeamini upo fea sanaa

trymjukuu: Safiii sana iwish cku mpge ngoma pamoja

tjhaniu: Hii inafanywa na wale tu wenye moyo safi.

d_mageziofficial: Sasa sina shaka kukuita legendary @therealfidq !! Huo ni utu uzima bro Endapo Fid Q na Joh Makini wakiamua kufanya wimbo wa pamoja au kufanya tour mikoani wakaandaa show za uwanjani naamini watatengeneza pesa ndefu sana.
Powered by Blogger.