Fans Wa Darassa Instagram Wamkataza Rapa Huyo Kutoa Ngoma Nyingine Kwasasa


Muziki imekua ni ngoma ya kihistoria katika maisha ya Darassa pamoja na Bongo Flava kwa ujumla kwa sasa. Naweza kusema ni ngoma ambayo imeishi muda mrefu na bado inazidi kufanya vizuri.

Haikuwa mategemeo yangu kuona watu watagoma kupokea kazi nyingine kutoka kwa mbabe huyo wa ‘Muziki’ ambaye ametumia ukurasa wake wa Instagram kuuliza kama mashabiki wake wapo tayari kupokea kazi mpya.

A photo posted by MagicMusicBoy #CMG (@darassacmg) on
 
“Any new about #muziki before to drop another bullet please?” Darassa ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hizi ni baadhi ya comments za mashabiki wake kuhusu post hiyo:

@susuliciousLbd utoe remix ya mzik lkn ngoma nyingne hatutak utuache kwanza ndo kwanza umetuingiza darasan ata pindi halijaanza

@mobdak_kessyBado kwakweli subiria kwanza,Maana mimi binafsi naona km umeutoa leo hamu bado haijaisha kila siku bado uko kwenye chart,sikushauri kwakweli

@msuyasaimonmkilimanjarowapekee Darasa tulia kidogo ndugu #muziki bado inabamba ndugu

@beyhvworldJuzi tulikua Kwenye graduu wimbo wa darasa umepigwa mara 7..but watu bado wanademand #muziki upigwe tena….jaman @darassacmg waachae kidogo na wenzako

@danfordboazBrother cjutiii kusikiliza ngoma tangia sikatitamaa adi now muziki xo now enjoy good life umetoka mbalisanaabroo nangoma zako kalii zotee, aiseee weka muziki maneno waachie wenyewee xo god bless mingiiiii kwakoooo bt tupe ngoma mpyaa.
Post a Comment
Powered by Blogger.