Fahamu Undani wa kilichoivuta Sprint kununua sehemu ya Tidal kwa $200m

Kampuni ya Sprint ilitangaza Jumatatu hii kuwa imenunua asilimia 33 ya share za Tidal, huduma ya kustream muziki ambayo rapper Shawn “Jay Z” Carter aliinunua mwaka 2015.

Mchongo huo umeripotiwa kuwa na thamani ya dola milioni 200, kwa mujibu wa tovuti ya Billboard. Kwa dau hilo, Tidal sasa ina thamani ya dola milioni 600, ambayo kiukweli ni faida kubwa na imemlipa Jay Z sababu yeye aliinunua huduma hiyo kwa dola milioni 56 kutoka kwenye kampuni ya Sweden, Aspiro, pamoja na huduma nyingine iitwayo WiMP.

Hata hivyo, thamani ya deal hilo imezua maswali mengi hasa kutokana na matatizo mengi yaliyopo Tidal tangu kuanzishwa kwake. Kuwa na wenyeviti watendaji 3 katika mwaka wake wa kwanza, utata wa umiliki wa nyimbo za Drake ambaye mwanzoni alisaini na Tidal, lakini akajiondoa siku mbili kabla ya uzinduzi wake na kwenda kusaini na Apple Music.

Pia, kuna kesi kibao, kuanzia ya CEO wa Cash Money Records, Birdman anayeshtaki Tidal over dhidi ya album ya Lil Wayne hadi kwa Carter kuwashtaki wamiliki wa mwanzo wa Tidal kuwa walidanganya idadi halisi ya watumiaji. Kuna shida pia ya Tidal kuahidi kuwa album ya Kanye West ingewekwa kwenye mtandao huo pekee hadi familia ya Prince kuishtaki Roc Nation kwa Tidal kustream muziki wa Prince bila ridhaa.

Hadi sasa, hakuna anayejua idadi kamili ya watumiaji wa Tidal. April mwaka jana, Tidal ilitangaza kuwa ina watumiaji milioni 3 wanaolipa na 45% kati ya wamejiunga na huduma ya malipo ya $20 kwa mwezi ili kupata muziki wenye kiwango cha juu zaidi.

May, Tidal ililiambia gazeti la New York Times kuwa ilipata watumiaji wapya milioni 1.2 katika wiki ya kwanza tangu album ya Beyonce, Lemonade iwekwe exclusively; na hivyo kufanya idadi ya watumiaji wanaolipa kufikia milioni 4.2.

Lakini kuna ripoti ya mwezi huu ya gazeti la Norway, DN.no iliyomshutumu Jay Z na Tidal kwa anadanganya idadi ya watumiaji. Ilidai kuwa, Tidal ilikuwa na watumiaji 850,000 tu ilipodai kuwa imefikisha watumiaji milioni 3. Na pia, Aspiro ilipoteza dola milioni 28 mwaka 2015 chini ya Jay Z.

Haya yote, yanazalisha maswali mengi kuhusu kwanini Sprint, inayomilikiwa kwa wingi na SoftBank, kuona kuwa deal la Tidal ni la maana. Kwanini itumie dola milioni 200 kumiliki theluthi moja ya huduma ya kustream muziki yenye watumiaji milioni 1 tu? Kwa kufananisha na wapinzani wake, Spotify sasa ina watumiaji milioni 43 wanaolipia huku Apple Music ikiwa nao milioni 20.

Jibu linapatikana kwa wamiliki 20 wa Tidal na ukuaji mkubwa wa huduma za kustream muziki. Ukimtoa Jay Z na mkewe Beyonce, wasanii wengine 20 wanamiliki hisa za kampuni hiyo wakiwemo Alicia Keys; Arcade Fire; Calvin Harris; Claudia Leitte; Coldplay; Daft Punk; Damian Marley; Deadmau5; Indochine; Jack White; Jason Aldean; J. Cole; Kanye West; Lil Wayne; Madonna; Nicki Minaj; Prince (familia yake); Rihanna; Cliff “TIP” Harris; na Usher.

Kila mmoja kati ya wasanii hawa 20, anamiliki 3% za Tidal ambayo inafikia 60% bila Jay Z na Beyonce, kwahiyo 66% ambayo Sprint haitokuwa chini yake, itamilikiwa na wasanii. Ni kama tu ambavyo Sprint inaelezea kwenye taarifa yake kwa waandishi wa habari, “Jay Z and the artist-owners will continue to run Tidal’s artist-centric service.”

Lakini nyongeza ya kupata “unlimited access to exclusive artist content not available anywhere else,” Sprint imewaongeza mastaa hawa kwenye familia yake.

 

Hivi ndivyo mambo huenda katika deals za muda mrefu kati ya makampuni ya habari ama ya teknolojia na mastaa wanaotengeneza maudhui. Mfano, angalia mkataba mpya wa Netflix na Jerry Seinfeld ama mkataba mrefu kati ya Adidas na Kanye West, au mkataba wa Intel na Will.i.am.

Kupata kipande cha umiliki wa Tidal, kunamaanisha kuwa Sprint inapata access kwa wasanii wanaomiliki Tidal, hiyo ina maana kuwa kuna uwezekano ikaanza kuwatumia katika kutangaza mambo yake. Tazamia tangazo la Sprint + Tidal likiwa na sura ya Rihanna hivi karibuni.

Faida nyingine kubwa kwa Tidal sasa zaidi ya fedha walizolipwa, ni kwamba watumiaji milioni 45 wa mtandao wa Sprint, wataendelea kulipia Tidal kama watataka kujiunga, lakini watapata exclusive mapema.

Na Sprint, ambayo ilipoteza nafasi yake ya 3 kwa T-Mobile mwaka jana miongoni mwa watumiaji wa simu Marekani, inahitaji watumiaji vijana ambao wataganda kwenye simu zao kwaajili ya burudani.

Hivyo licha ya wachambuzi kudai kuwa kuwa Tidal haiwezi kuwa na thamani ya $600m, bado Sprint itapata faida ya kuwa karibu na nyota 21 wakubwa itakaowatumia itakavyo.
 0
Source: Yahoo Finance
Powered by Blogger.