Everton Kumsajili Mchezaji Huyu Kutoka Algeria

Image result for Ishak Belfodil

Klabu ya Everton imekubali mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Algeria na klabu ya Standard Liege Ishak Belfodil.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anatarajiwa kuelekea Mersyside kufanyiwa ukaguzi wa matibabu.
Mchezaji wa Manchester United Morgan Schneiderlin pia alifanyiwa ukaguzi huo katika klabu hiyo siku ya Jumatano.
Related image

Kiungo huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 27 anatarajiwa kugharimu hadi pauni milioni 24. Everton tayari imemsajili mshambuliaji wa Charlton Athletic Ademola Lookman mwenye umri wa miaka 19 kwa kitita cha pauni milioni 11 mwezi huu.

Belfodil ambaye hakujumuishwa katika kikosi cha Algeria kitakachoshiriki katika kombe la mataifa ya Afrika, kwa sasa anafanya mazoezi na Standard Liege nchini Uhispania.

Amejiunga na klabu hiyo msimu huu na amekuwa na mafanikio makubwa baada ya kuichezea Lyon, Bologna, Parma, InterMilan, Livorno na Baniyas katika mataifa ya miliki za kiarabu.
Post a Comment
Powered by Blogger.