It's Thursday Let's ThrowBack Na Hii "El Chapo Ya @AyTanzaniaTangu August 2016 El Chapo ya Ay imekuwemo kwenye list yangu ya ngoma kali za Rapa AY, Kinachonifanya niipende ngoma hii sio tu ubora wa Audio wala Video Production yake. 

Kupitia "El Chapo" AY amejivunia mafanikio yake na hatua kibao anazopitia. Ni kweli AY ni mkongwe kwenye game na bado anafanya maajabu makubwa, huenda ukali wake wa Flows AY umemfanya kuwa ni mwanamuziki wa kwanza kutoka Tanzania kufanya kolabo kubwa na wasanii wa nje akiwemo Romeo, Miss Trinity, Lamaya na Sean Kingston. 

Sitaingia kiundani sana kumuhusu AY, lakini naungana na Kauli yake Iinayosema..

"Rule Namba moja yangu ni kuishi tu peace, Naishi maisha yangu bila mtu kumplease, 
sipendi kabisa ku-entertain shit".

Kinachofanya niungane na AY kwenye kauli yake hiyo hata wewe unaweza kuwa shahidi wa hili. AY ni mmoja kati ya wanamuziki wanaotajwa kuwa na mafanikio makubwa kibongo bongo lakini binafsi yeye mwenyewe hajawahi kuyaweka wazi mafanikio yake.

Kingine ambacho AY amefanikiwa kuwa nacho ni kuepuka skendo za Magazeti na mitandao ya kijamii, Kifupi AY sio mtu wa drama.  

Lugha iliyotumika kwenye El Chapo ni lugha rahisi kabisa ambayo mtu yeyote anaweza kusikiliza na kufurahia muziki huo

Enjoy NaYO hapa


Powered by Blogger.