Dully Skyes Adai Kwasasa Amekuwa Mtu Mzima Na Hataki Kuona Akichafuliwa Jina


Mwanamuziki mkongwe kwenye muziki wa bongo fleva Dully Skyes, ambaye hivi sasa anatamba na wimbo wake ‘Yono’ amefunguka na kusema yeye amekuwa mtu mzima hivyo haitaji kuchafuliwa kwa kuzushiwa mambo ambayo yeye hajayazungumza.

Dully Skyes alisema hapendi kuona watu wanaandika vitu vya uongo kuhusu yeye ambavyo vinakuwa na lengo la kutaka kumchonganisha na wasanii wa sasa ambao wengi wao ni wadogo zake na kusema yeye mwenyewe anawategemea sana wasanii hao.

“Bloggers jamanii naombeni muwe mnaandika vitu ambavyo mnavisikia kwenye Interview na si kuandika vitu vya uongo uongo, manake nimesikia juzi kati hapa wameongea juu ya Darassa sijui nimesema Darassa sijui nini na nini ni uongo huo, wasiongee vitu vya uongo wanatuma vitu Instagram lakini hawaongei vitu wanavyovisikia hapa, wanaleta chumvi chumvi ili wapate sponsers kutumia uongo”. Alisema Dully Skyes kwenye kipindi cha Planet bongo.

Mbali na hilo Dully Skyes aliwaomba bloggers kutomgombanisha na wadogo zake kwenye muziki kwa kuwa yeye mwenyewe anawategemea hao wasanii kwani kuna vitu vingi yeye hawezi kuviona lakini wao wakaona na kumpa njia nzuri ya kupita.

“Jamani mimi nishakuwa mtu mzima sihitaji kuchafuliwa hao kina Darassa, kina Mr Blue kina nani ni wadogo zangu hao na mimi nawategemea wao, mimi sasa hivi sina njia wala sina jicho kuona lakini wao wanaona mengi sababu ndiyo vijana wa kileo kwa hiyo nawategemea wao msinigombanishe na wadogo zangu”alisema Dully Skyes.
Post a Comment
Powered by Blogger.