Drama: Roma Awataka Madee Na Nay Wa Mitego Kutamka Neno 'Manzese' Kisha Atoe Suluhisho Hili


Kumekuwa na kile wengi huita "Kiki" kutokana na wote wawili kuwa na kazi zao tayari zishaingia uraiani. Mapicha picha ya hawa wawili yamekuwa kila siku yakitengeza sura mpya huku jambo hilo linadaiwa kuanza pale baada ya Madee kuachia ngoma yake mpya "Hela".

Ngoma ya Madee "Hela" ambayo imetafsiriwa kumwendea hasimu wake, Nay, kupitia mstari unaosema “Yule kijana wa home sio staa, anatukana hata waliomzaa, wivu tamaa na njaa ukiendekeza ujue kidole utakaa,” Madee amerap kwenye ngoma hiyo.Baada ya muda mfupi tangu wimbo huo utoke, Nay aliandika kwenye Instagram, “Leo nimesikia Wimbo Mbayaaaaa kuliko nyimbo mbaya nilizowahi kusikia Mwaka huu.” “Mtag uyo Msanii mwenye huo wimbo Kama ushausikia..?!”

Hali hiyo ikapelekea kuwepo kwa U-HEARD kuhusu jambo hilo kwenye XXL ya Clouds Fm. GossipCop wa segment hiyo Soudy Brown, alimuuliza kuhusu post yake hiyo kama amemlenga Madee au lah!

Nay wa Mitego alikanusha vikali tuhuma hizo na kudai kwamba hajawahi hata kuusikia wimbo huo.

Leo Kupitia nstagram ya Roma, alipost ujumbe huu kuhusu Madee & Nay Wa Mitego. Ujumbe huo ulionekana kama hivi..

 

 Ujumbe huo ulisomeka hivi "Oyaaaaah!! Sililizeni Nyie Mnatuchosha Bana na Vimaneno maneno vyenu kila saa kwenye Radio Zetu....Ili Mradi tu Mvikikishe #vinyimbo vyenu mlivyoachia!!! Mbona #Sisi_Tumetulia_tu. Na tumeachia Dude. #SASA_NASEMAJEEEEE Nyie Si Mnaigombania #MANZESE!!??? Sasa nataka Nyote wawili @madeeali @naytrueboy Mlitamke hilo neno #MANZESE atakayelitamka vizuri kwa kulipatia ndio MWENYE MANZESE YAKE.Aaaaf Andaeni #Pambano mimi #Refa"
Post a Comment
Powered by Blogger.