Ditto Afunguka Mipango Yake Ya Kuachia AlbamuMsanii wa bongo fleva pia ni hit maker wa wimbo ‘Moyo Sukuma Damu’ Lameck Ditto amesema anajipanga kurudi na mfumo wa kuachia albamu ya nyimbo zake mwishoni mwa mwaka huu japo haijazoeleka kwa wasanii wa Tanzania.

Kwa sasa wasanii wengi wa muziki Bongo wamekuwa na msukumo mkubwa wa kuachia albamu huku Navy Kenzo wakiwa wamefungua njia hiyo baada ya kufungwa kwa miaka mingi.

Uamuzi huo wa kutoa albamu unamfanya awe ameungana na wazo la kundi la muziki la Navy Kenzo, ambao pia mwishoni mwa mwaka jana walitangaza kuja na albam ya ngoma zao inayokwenda kwa jina la AIM.

 

 Akiongea kupitia eNewz Ditto amesema kwa sasa anaendelea kurekodi nyimbo nyingi ili hapo baadaye aweze kuchagua ni zipi ambazo zinafaa kukaa kwenye albamu yake ingawa kwa sasa ataachia nyimbo mbalimbali ili kuweza kurudisha mashabiki zake na kurudisha hadhi yake ya zamani.

Pia Ditto amesema kwa sasa anajipanga kutengeneza utamaduni wake na akifanikiwa kwa hilo atajiingiza kwenye biashara za kuachia albamu mbalimbali na pia amewashukuru mashabiki kwa kuupokea vyema wimbo wake wa moyo sukuma damu.
Post a Comment
Powered by Blogger.