Dimitri Payet Aondolewa Kundi La WhatsApp, Adaiwa Kuwa Msaliti


Mikasa ya kutengwa imeendelea kumuandama kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa Dimitri Payet, kufuatia sakata la kushinikiza auzwe katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Payet ameendelea kukutwa na madhila hayo, baada ya kufutwa kwenye kundi la WhatsApp la wachezaji wa West Ham.

Kitendo hicho kimetafsiriwa kama wachezjai wa West Ham Utd wamechoshwa na mwenendo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye ameendelea na msimamo wake wa kutaka kuondoka klabuni hapo.

Ufukunyuzi uliofanywa na gazeti la The Sun umebaini kuondolewa kwa Payet katika kundi hilo, kumetokana na kuonekana kama msaliti ambaye hapaswi kuwa sehemu ya wachezaji wengine, ambao wamejitoa kwa moyo mmoja kuitumikia West Ham Utd.

Kabla ya hapo nahodha na kiungo wa West ham Utd Mark Noble, aliotangaza hadharani kuvunja uhusiano wa kirafiki na Payet, kwa kigezo cha kuchoshwa na mwenendo wake wa kushinikiza kuondoka kwa kugomea mazoezi pamoja na mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita.

Tayari klabu ya Olympic Marseille ya nchini Ufaransa imeshaonyesha nia ya kutaka kumsajili Payet kwa kutuma ofa, lakini ilikataliwa na viongozi wa West Ham Utd ambao walisisitiza kuwa katika mazungumzo ya kumshawishi Payet abadili msimamo wake.

Taarifa nyingine zimeeleza kuwa, baadhi ya viongozi wa klabu hiyo ya jijini London, wameafiki kuuzwa kwa kiungo huyo kwa sharti la kupokea ofa isiyopungua kiasi cha Pauni milioni 30.
Post a Comment
Powered by Blogger.