Diamond Aweka Wazi Mpango Wake Wa Kufanya Kolabo Na Msanii Kutoka Colombia, Shakira


Ukiachana na Kolabo alizofanya mwaka jana Diamond Platnumz bado hajapunguza kasi ya kolabo na mwaka huu kolabo zake nyingi zitakuwa ni za kimataifa zaidi tena kuvuka Bara la Afrika.

Diamond Platnumz kupitia Insta Live amesema mwaka huu atafanya Kolabo na msanii maarufu Duniani kutoka Colombia Shakira na pia kama haitoshi kathibitisha wimbo wake wa I miss u remix aliofanya na Jahpraiz kutoka Zimbabwe kuwa upo tayari na video imeshafanyika anasubiri uongozi tu kuutoa.Mbali na hilo pi lile la Chibu Perfume za mkali wa wimbo Salome, Diamond Platnumz zitaingia sokoni muda wowote kuanzia sasa.

Mwaka 2016 muimbaji huyo alionyesha sample ya perfume hizo hali ambayo ilileta shauku kubwa kwa mshabiki wa muimbaji huyo.
Post a Comment
Powered by Blogger.