Diamond Aweka Rekodi Hii Mpya Youtube Kupitia Wimbo Wake Wa ‘Nana’


Diamond Platnumz ni moja ya wasanii wakubwa Barani Afrika kwani mbali na Tuzo za kimataifa anazokwara kila kukicha lakini pia tumeona kazi zake zinavyopokelewa vizuri hata kwenye matamasha tumeona nyomi anazojaza.

Sasa kupitia wimbo wake wa Nana ambao amemshirikisha Mr Flavour ameweka Rekodi ya Video yake ya kwanza kufikisha Views Milioni 20 huku wimbo huo ukiwa na Mwaka Mmoja na Miezi 8 tu,mbele ya wimbo wake wa Number One Remix yenye Views Milioni 19 ambayo ina miaka mitatu mpaka sasa.


Na mpaka sasa video ya Bongo Fleva iliyotazamwa zaidi ni ya wimbo wa ‘Sugua Gaga’ wa Shaa ambao una Views Milioni 21 hivyo tusubirie kuona Rekodi hiyo ikivunjwa mwaka huu.


Post a Comment
Powered by Blogger.