Deal Done: Philippe Countinho Ajitia Kitanzi Hadi 2022

Kiungo mshambuliaji kutoka nchini Brazil na klabu ya Liverpool, Philippe Coutinho amesaini mkataba mpya, ambao utamuwezesha kubaki Anfield kwa miaka mitano ijayo.

Taarifa zinasema katika mkataba huo mpya Coutinho atakuwa akilipwa kiasi cha paundi laki moja na nusu kwa wiki na kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa kwenye klabu ya Liverpool.

Coutinho amesema ameamua kubaki Liverpool kwa sababu ni klabu inayompa furaha moyoni mwake na mashabiki wake wamekuwa wakimuunga mkono tangu ajiunge nayo.

Nyota huyo amekuwa mtu muhimu sana chini ya meneja Jurgen Klopp na amekuwa msaada tosha kwa timu hiyo kwenye harakati zake za kuwania ubingwa wa England msimu huu huku akiwa amefunga magoli 34 ndani ya michezo 163 aliyoichezea tangu alipotua Anfield Januari 2013.
Powered by Blogger.