Dani Carvajal Aumia, Yadaiwa Atakaa Nje Kwa Mwezi MmojaBeki wa pembani wa mabingwa wa soka duniani klabu ya Real Madrid Dani Carvajal, huenda akaukosa mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Società Sportiva Calcio Napoli.

Beki huyo kutoka nchini Hispania amekadiriwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha mwezi mmoja, kufuatia majeraha ya nyama za paja, ambayo aliyapata akiwa katika mazoezi siku ya jumanne.

http://i1.wp.com/dar24.com/wp-content/uploads/2017/01/Dani-Carvajal01.jpg?resize=738%2C415

Kwa makadirio hayo, beki huyo mwenye umri wa miaka 25 anategemea kukosa michezo mitano ya ligi ya nchini Hispania (LaLiga) michezo ya kombe la Mfalme (kama watafanikiwa kuitoa Celta vigo) pamoja na mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Michezo ya ligi ambayo Carvajal ataikosa itakua dhidi ya Malaga, Real Sociedad, Celta Vigo, Osasuna pamoja na Espanyol.

Hata hivyo beki mbadala Danilo anategemewa kuziba pengo la Carvajal, na kama itashindikana bado Zidane atakuwa na chaguo la kumtumia Nacho au Sergio Ramos.
Post a Comment
Powered by Blogger.