Country Boy Aiweka Wazi Kolabo Anayoikubali Zaidi


Rapa Country Boy amefunguka na kuitaja ngoma ya 'Hakuna matata' ambayo ameshirikiana na Bill Nas kuwa ndiyo 'kolabo' anayoikubali na kuilewa zaidi tangu ameanza kufanya muziki.

Country Boy  alisema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo na kusema wimbo huo ni moja ya ngoma anayoikubali zaidi tangu ameanza kufanya kazi na kushirikiana na wasanii wengine na kusema anaupenda wimbo huo kwa kuwa una ujumbe ndani kuwa hata watu wakibana vipi mdogo mdogo watasonga na kufikia malengo.


Mbali na hilo Country boy amedai kwa sasa anajipanga kuachia video ya wimbo huo ambayo huenda ikatoka mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi wa pili.
Powered by Blogger.