Country Boy Afunguka Haya Baada Ya Kujiunga Na 'Live First Live Good'


Msanii wa bongo fleva Country Boy amesema ameamua kujiunga rasmi na Petit Man chini ya meneja Mchafu  kwa mwaka 2017, ili kuweza kutangaza muziki wake Kimataifa zaidi.Country Boy amesema ameamua kujiunga  na 'lebo' ya 'Live First Live Good' kwa mwaka huu kwa kuwa ni menejiment iliyokuwa ikimsapot chini kwa chini tangu zamani huku wakimpa 'chance' ya kumchunguza kwa upande wa nidhamu na amesema anajisikia furaha kujiunga na lebo hiyo, alisema Country Boy kupitia eNEWZ.

Hata hivyo Country Boy amesema hiyo ni lebo ambayo imeweza kumtoa msanii Bill Nass kupitia ngoma ya Chafu Pozi na muziki wake kufanya vizuri hivyo anaamini yupo kwenye mikono salama na muziki wake utafika mbali zaidi.
Post a Comment
Powered by Blogger.