Country Boy Aelezea Sababu Za Kuja Na Muonekano Mpya


Kama unamfuatilia kwa ukaribu Rapper Country Boy, basi utakuwa umeona utofauti alionao kwa sasa kimuonekano kuanzia nywele na namna anavyovaa.


katika harakati zakumtafuta Country Boy kutaka kufahamu kilichomfanya abadilishe muonekano wake.

Country Boy alisema “Unajua mimi ni msanii ambaye kwanza napenda identity, yaani napenda muonekano wangu uwe rahisi kunitambua. Niko tayari nijitofautishe na watu wote nikaonekana kama mshamba, lakini still huo huo ushamba wangu ambao pengine mtu anaweza akacheka kwanini navaa vile lakini ile ni identity kwamba ukiniona tu utacheka, that’s Me".

Country Boy ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya Hakuna Matata aliyomshirikisha Bill Nas,amedai kuwa anajivunia kubuni style za nywele na mavazi ambazo watu wengi wamekua wakiziiga.
Post a Comment
Powered by Blogger.