Copa del Rey: FC Barcelona Watamba Mbele Ya Real Sociedad

Mabingwa wa soka nchini Hispania (FC Barcelona), wametinga kwenye hatua ya nusu fainali ya kombe la Mfalme (Copa del Rey) kwa kishindo, baada ya kuibanjua Real Sociedad.

FC Barcelona walipata ushindi mnono wa mabao matano kwa mawili wakiwa katika uwnaja wao wa nyumbani Camp Nou, na sasa wanajiunga na Celta Vigo, Atletico Madrid pamoja na Alaves kwenye hatua ya nusu fainali.

Mabao ya FC Barcelona yalifungwa na Denis Suarez, 17′, 82′, Lionel Messi 55′, Luis Suarez 64 na Arda Turan 84′ huku mabao ya  Real Sociedad yakikwamishwa kimiani na Juan Miguel Jiménez López 62′ na Willian Jose 73′.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza FC Barcelona walichomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri.
Kwa mantiki hiyo FC Barcelona wametinga nusu fainali kwa jumla ya mabao sita kwa mawili.

Shirikisho la soka nchini Hispania linatarajiwa kupanga ratiba ya nusu fainali ya Copa del Rey, na kuna wasiwasi kwa FC Barcelona kukutana na Atletico Madrid.
Powered by Blogger.