Al Shabaab yadai kuua askari wa Kenya

 kikundi cha kigaidi la nchini SOMALIA AL SHABAB limesema wapiganaji wake wameua vikosi vya askari wa Kenya walivyovivamia katika eneo la kificho katika kambi ya jeshi

Kundi la kigaidi la nchini SOMALIA AL SHABAB limesema wapiganaji wake wameua vikosi vya askari wa Kenya walivyovivamia katika eneo la kificho katika kambi ya jeshi iliopo kusini mwa nchi hiyo, dai ambalo limepingwa na jeshi la KENYA.

Msemaji wa kikundi hicho, ambacho kimekuwa kikishambulia vikosi vya UMOJA WA AFRIKA vilivyopo katika pembe ya nchi hiyo ya AFRIKA, alisema kuwa  siku ya IJUMAA wapiganaji wake waliua wakenya 57 katika kambi iliyoko katika mji wa KULBIYOW siku moja kabla.

Mbali na kufanya mauaji hayo kundi hilo pia limedai kuishikilia kambi hiyo inayoendeshwa na MPANGO MAALUM WA UMOJA WA AFRIKA NCHINI (AMISOM) SOMALIA.

Mwezi Januari mwaka uliopita, al Shabab ilisema imeua zaidi ya wanajeshi wa Kenya 100 huko EL ADDE, kambi ya SOMALIA iliyopo karibu na mpaka wa KENYA, taarifa ambayo ilipuuzwa na JESHI LA KENYA, huku vyombo vya habari vya KENYA vikiripoti na kutoa idadi ya wanajeshi waliouawa.Chanzo: TBC
Powered by Blogger.