Bill Nas Kilitaka Kumkuta Cha Kiba Na Diamond, Msikie Hapa Akifunguka


Inavyodaiwa kuwa chanzo cha bifu kati ya Diamond Platnumz na Alikiba kilianzia kwenye wimbo baada ya msanii mmoja kufuta mistari ya msanii mwingine katika wimbo alioshirikishwa, jambo hilo pia lilitaka kutokea kwa Rapa Bill Nas.

Hiyo ni baada ya kusikia Mwana FA amechana katika wimbo wake wa "Mazoea" bila kumpa taarifa, jambo lililomfanya kutaka kufuta mistari yake, ili ubaki kuwa ni wimbo wa Mwana FA bila yeye kushiriki. 

Bill Nas alidai kuwa hakupanga kufanya kazi hiyo na Mwana FA bali Mwana FA aliisikia ngoma hiyo na kuamua kuifanya bila kumpa taarifa Bill Nas.


"Mwana FA alini'suprise' mimi nakumbuka nilimtumia demo ya kazi, yeye aliandika mistari na kwenda kwa Harmy B akiingiza sauti kisha wakaenda mpaka kwa Mr T Touch na kufanya bila kunipa taarifa, siku hiyo nipo studio ndiyo wananisikilizisha kiukweli nilifurahi sana ila baada ya hapo baada ya kusikia ile mistari nikaona hapana ngoja nifute verse zangu ili niingize tu melodies maana Mwana FA alikuwa amechana sana, lakini Mr T Touch alikataa" alisema Bill Nas kwenye Planet Bongo.

Mbali na hilo Bill Nas anasema wimbo wake huu wa 'Mazoea' ni wimbo ambao ulikuwepo muda mrefu kabla ya Ligi ndogo, na Chafu pozi 
Powered by Blogger.