Ben Pol: Thamani Ya Sauti Yangu Ni Zaidi Ya Milioni 10


Mkali wa wimbo wa ‘Moyo Mashine’ , Benard Paul  (Ben Pol), ameweka wazi kwamba  msanii ambaye hajafikia kiwango chake na anataka kumshirikisha katika wimbo wake, awe ameandaa milioni 10 ama amwachie fedha za malipo atakayoingiza kupitia Youtube na miito ya simu.
Mazingira hayo magumu ya msanii huyo yanawalenga wasanii wanaochipukia, huku wale wenye majina makubwa akiwemo Ali Kiba, Diamond, Vanessa Mdee, Nevy Kenzo, Jux na AY akidai kwamba hawatuhusishwa na fedha hizo kwa kuwa wapo  katika mpango wa kuafanya nao kazi.

 ”Wasanii wenye majina na sijashirikiana nao hawataguswa na hizo millioni 10 lakini wengine tutazungumza inaweza, isifike hiyo fedha kama ntaona manufaa katika kolabo hiyo.
”Kama unaamini wimbo wako ni mzuri na unajua siwezi kukataa tutazungumza tofauti ya kunipa milioni 10, unaweza kuniachia malipo ya youtube na ‘ring tone’ (miito ya simu) za huo wimbo ama makubaliano mengine” ameeleza Ben Pol.
 
Ben Pol & AY

Mbali na hilo, hapa majuzi AY alimpaisha Ben Pol kwa kumpa sifa ya kuwa yeye ni R Kelly wa Afrika, R Kelly ni muimbaji wa R&B maarufu huko Marekani, huenda ikawa sababu ya Ben Pol kupandisha thamani yake katika kazi zake za muziki.
Post a Comment
Powered by Blogger.