Ben Pol Na Tiddy Hotter Watuhumiwa kumuibia Beat Na Chorus Ya ‘Phone’, Producer Huyu Kutoka Kenya


Producer Sappy mwenye makazi yake nchini Kenya na anayefahamika kwa kutayarisha nyimbo za mastaa kadhaa zikiwemo XO ya Joh Makini na nyimbo nyingi za Redsan, amewatuhumu Ben Pol na producer wa wimbo wake mpya, Tiddy Hotter kuwa wamemuibia idea ya beat yake pamoja na chorus ya wimbo huo uitwao ‘Phone.’

 Sappy ni producer anayetokea Mwanza lakini amehamishia makazi yake jijini Nairobi, Kenya na kwa sasa ni miongoni mwa watayarishaji wakubwa wa huko

Kwenye wimbo huo Ben amemshirikisha msanii wa Ghana, Mr Eezi.

Sappy anadai kuwa baada ya kuusikia wimbo huo wa Ben Pol na kugundua kuwa beat na chorus ya msanii aliyekuwa aitumie aitwaye Ervixy Kalla ambaye ndiye mtunzi wa kionjo cha chorus hiyo vinafanana na Phone, aliwasiliana na Tiddy na Ben Pol ambao anadai hawakumpa ushirikiano.

Akiongea  na tovuti ya Bongo5, Sappy alisema “Hiyo ngoma mimi niliifanya toka last year, nilifanya na msanii wangu anaitwa Ervixy, na studio niliyokuwa natumia ni ya Tiddy Hotter, alikuwa na studio Mwanza kipindi hajahamisha studio Dar,”.

 Ervixy Kalla ni msanii wa Sappy ambaye ndiye mtunzi wa kionjo cha chorus kinachosikika kwenye wimbo Phone wa Ben Pol

Sappy anasema mara nyingi alipokuwa Mwanza alikuwa akimlipa studio time Tiddy ili arekodi na wasanii wake.

“Nimeshangaa kitendo kwamba watu wanafanya ngoma bila idhini za watu. Tena hiyo chorus imeiambwa exactly kabisa na sisi tulivyoifanya, yaani hakuchenji kitu chochote, melody kila kitu amefanya exactly kabisa,” amesisitiza.

  
Tiddy ni miongoni mwa watayarishaji wakubwa wa Bongo na ndiye aliyetayarisha wimbo wa Belle 9, Burger Movie Selfie

Sappy anadai kuwa kama Ben Pol na Tiddy wangeonesha ushirikiano alipowagia simu wangeyamaliza kiume, lakini amelazimika kuiweka hadharani ili watu waujue ukweli. “Issue kubwa hapa ni kuwa hawajatuomba hiyo ngoma na kupata idhini yetu, that’s is unprofessional, mimi sikupenda kitu kama hicho kabisa.”

Kwa upande wake Ervixy aliyekuwa mmiliki wa kwanza wa idea hiyo ameandika kwenye Instagram: Shame on you @newtiddyhotter ..Nani akuchafue unajua nidham ya undugu we we…njaa za masaa zinakuponza huwezi kaa poa na niggas,,una act like ujui…ongea ukweli kipi ukijui.. #phoneiambenpoul #phoneervixy na wewe ndo mtu kati mnafiki na utakimbia kila msehem #snich*ssniggah ukwel utajulikama tu.”

Naye Tiddy ambaye kwa sasa yupo Zanzibar na Ben Pol na Mr Eazi walikoenda kwenye kile kinachoonekana kama kushoot video ya wimbo huo, ameiambia Bongo5, “Sijawahi kuiba idea, u know me, na sitokuja kutumia idea ya mtu.”

-Bongo5
Post a Comment
Powered by Blogger.