Ben Pol Anyoosha Maelezo Baada Ya Ngoma Yake 'Phone' Kujibiwa Na Mbunge


Unaposikia msanii kaamua kumjibu msanii mwenzake mara nyingi huwa ni kawaida, lakini unaposikia Mbunge wa Bunge la Tanzania ameamua kuingia studio na kujibu ngoma fulani, hapo lazima utatamani kujua pia ilikuaje na alifikiria nini.

Ukizingatia jina la Mbuge huyo halijawahi kuonekana kwenye ramani ya muziki wa Bongo Fleva. Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya ameamua kuingia studio na kumjibu Ben Pol ngoma yake ya "Phone".


Kupitia XXL ya Clouds Fm Jan 17, ilimpata Ben Pol ambaye aliweza kufunguka na kudai kuwa "Kilichotokea Mh aliandika mashairi ya kujibu phone halafu akatafuta namba yangu ya simu kisha akanipigia, akanambia Ben Pol napenda muziki wako, nyimbo zako pia unazoshirikishwa. Akaniambia kuwa nimeandika mashairi ya kuujibu wimbo wako mpya wa phone. Nataka nikusomee uyasikilize then ikiwezekana tuonane nikupatie then umpatie msanii yeyote wa kike anayeweza kuyatendea kazi".

Ben Pol aliongeza "Nikasikiliza the way alivyokuwa anayasoma nikaona yamekaa vizuri, nilivyokuja kuonana naye nikamwomba a-record yeye badala ya kumtafuta msanii mwingine. Nikamwambia unaweza kuifanya kama mashairi, tukaifanya kama ushairi akakubali. Tukafanya arrangement then tukairecord. Mh aliridhika kui-record mwenyewe nikasema hii ni poa zaidi".

Sikiliza Mbunge Ester Bulaya alichomjibu Ben Pol kwenye ngoma yake ya PhonePost a Comment
Powered by Blogger.