Ben Pol Afunguka Kuhusu Kolabo Yake Na Chidinma Kuchelewa Kutoka


Hit maker wa Moyo Mashine ambaye kwa sasa anafanya vizuri kupitia wimbo wake wa "Phone", amefunguka kuhusu ujio wake unaosubiriwa kwa hamu kubwa na msanii kutoka Nigeria.

Kwenye ahadi ambazo Ben Pol aliwahi kuzitoa mwaka 2016 ni kolabo yake na mwanadada kutoka Nigeria Chidinma na aliahidi kolabo mbili moja ilikua ni rmx ya wimbo wake wa Moyo Mashine na nyingine ilikua ni ngoma nyingine mpya ambayo haikurekodiwa na ahadi hii aliitoa mwezi Mei 2016.

Akiongea kwenye XXL ya Clouds Fm Ben Pol amesema"Chidinma amefanya nyimbo mbili Moyo Mashine remix na wimbo mwingine,moyo mashine remix tulichelewa timing kwasababu plan ni kwamba remix iwe tayari kabla ya original haijatoka lakini tukachelewa timing".


Ben Pol aliongeza "Alikuja kuituma part yake kama sikosei Nov 2016 sasa Nov unafanyaje,utoe remix Nov ikawa siyo kweli,Sasa hivi niko naangalia,kwa sababu pia hatukuweza ku-shoot moyo mashine remix naangalia uwezekano wa ku shoot hiyo ngoma nyingine tuliyofanya".

Kuhusiana na ngoma yake mpya ya "Phone", Ben Pol amedai kuwa vipande vya Mr. Eazi vimeshakamilika ila bado vya upande wake tu kukamilisha na amechelewa kukamilisha kwa sababu kipindi kilichopita alikua busy sana na shows.
Post a Comment
Powered by Blogger.